Yanga kuwaongezea nguvu Job, Bacca, Mwamnyeto

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Dec 2024
Yanga kuwaongezea nguvu Job, Bacca, Mwamnyeto

Baada ya kutambulisha usajili wa mlinzi wa pembeni Israel Mwenda, Yanga pia inatarajiwa kufanya maboresho mengine eneo la beki wa kati

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said yuko sokoni kusaka beki mwingine wa kati mzawa ili kuwaongezea nguvu Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Dickson Job

Kwa sasa Yanga inalazimika kuongeza mlinzi mwingine wa kati hasa baada ya eneo hilo kuyumba katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita

Baada ya Bacca 'kula umeme' na Job kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano, Yanga ililazimika kucheza dhidi ya Tabora United na mlinzi wa kati mmoja tu, Bakari Nondo Mwamnyeto kufuatia Aziz Andabwile ambaye kocha wa zamani wa Yanga Miguel Gamondi alikuwa akimtumia kwa dharura katika safu ya ulinzi kupata majeraha katika mchezo huo

Yanga ililipa gharama ya uhaba wa mabeki wa kati ikizawadiwa kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Tabora United ukiwa ni mchezo wa pili mfululizo kupoteza kwenye ligi msimu huu baada ya kufungwa na Azam Fc

Mazingira kama hayo yakajitokeza tena katika dakika 10 za mwisho katika mchezo dhidi ya Namungo Fc baada ya Job kupata majeraha na kumlazimu Duke Abuya kumaliza mechi akiwa beki wa kati sambamba na Mwamnyeto

Beki wa Coastal Union na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Lameck Lawi na beki wa Fountain Gate ambaye pia huitumikia timu ya Taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes' Laurian Makame ni miongoni mwa majina yanayotajwa kuwa mezani kwa Injinia Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’