Yanga yaweka kando rekodi mechi dhidi ya TP Mazembe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Dec 2024
Yanga yaweka kando rekodi mechi dhidi ya TP Mazembe

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji watahitaji kupambana na kuvuja jasho jingi katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe ili kufufua matumaini ya kusonga mbele hatua inayofuata katika michuano hiyo

Yanga ilitua Lubumbashi jana tayari kwa mchezo dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa Jumamosi, Disemba 14 saa 10 jioni katika dimba la Mazembe

Kamwe amesema licha ya kuwa na rekodi nzuri ya ushindi katika mechi mbili za mwisho walizocheza dhidi ya TP Mazembe, ni juhudi na kujituma kwa wachezaji pekee ndiko kutawapa matokeo mazuri katika mchezo huo na sio rekodi

"Hatufikirii rekodi ya mechi zilizopita, hapa tulipofika hakuna rekodi yoyote inayoweza kutusaidia, kitakachotusaidia ni kuvuja kwa jasho letu kwenye mchezo huo, hakuna muda kutafuta vijisababu vya pembeni, ni muda wa kwenda kutokwa machozi, jasho na damu ili tupate matokeo mazuri"

"Ni mechi ngumu, lakini hakuna namna ni lazima tuikabili, tuna imani tunaweza kupata matokeo mazuri dhidi yao, malengo yapo pale pale, kufuzu kwenye hili kundi, haijaisha na wala hatujachoka," alisema Kamwe

Misimu miwili iliyopita timu hizo zilikutana mara mbili kwenye hatua ya makundi, Kombe la Shirikisho Afrika na Yanga kushinda michezo yote miwili, ikiichapa TP Mazembe mabao 3-1 Februari 19, mwaka jana Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na marudiano kushinda 1-0 kwenye uwanja wa ugenini

Mchezo huo wa kesho utazikutanisha timu ambazo hazijapata ushindi wowote kwenye michezo iliyopita katika kundi lao. Hata hivyo, TP Mazembe ina pointi moja iliyoipata kwa kutoa suluhu dhidi ya MC Alger ya Algeria, nyumbani, huku Yanga ikipoteza michezo yote miwili ya mwanzo kwa mabao 2-0 dhidi ya Al Hilal Omdurman ya Sudan na 2-0 dhidi ya MC Alger

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
3h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’