Hans Poppe ameunganishwa kesi ya akina Aveva

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 May 2018
Hans Poppe ameunganishwa kesi ya akina Aveva
Jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewaongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Pope na mkandarasi wa uwanja wa klabu hiyo, Frank Peter Lauwo katika kesi ya utakatishaji fesha na kugushi inayowakabili Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Mahakama hiyo, imeagiza Hans Pope na Lauwo wakamatwe na kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili.

Amri hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wa mahakama hiyo baada ya Swai kudai amewatafuta washitakiwa hao wamekuwa wakitafutwa tangu Machi mwaka huu bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata.

Kufuatia mabadiliko hayo washtakiwa, wamesomewa upya hati ya mashtaka na wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 10 tofauti na hati ya mashitaka ya awali iliyokuwa na mashtaka matano.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Leornad Swai amedai kwamba, kesi hiyo jana ilitajwa kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa hao maelezo ya awali, lakini ameomba kufanywa mabadiliko ya hati ya mashitaka.

Katika mashitaka hayo, washitakiwa wanakabiliwa na shitaka la kula njama, kutoa nyaraka za uongo, matumizi mabaya ya madaraka, kughushi, utakatishaji, kuwasilisha nyaraka za kughushi na kuendesha biashara bila kufuata sheria.

Akisoma mashitaka hayo, Swai amedai kwamba, katika shitaka la kwanza, Aveva na Nyange, walikula njama ya kutenda kosa la kutumia madaraka vibaya na kati ya Machi 10 na 16 jijini Dar es Salaam, walitumia madaraka yao vibaya.

Machi 15 mwaka 2016 wanadaiwa kuandaa fomu ya maombi ya kuhamisha dola za Kimarekani 300,000, karibu Sh. Milioni 700 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyopo CRDB tawi la Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Barclays kwa madhumuni ya kujipatia faida.

Aidha, wote kwa pamoja waliwasilisha nyaraka ya kughushi, inadaiwa kuwa Aveva Machi 15, 2016 katika banki ya CRDB aliwasilisha nyaraka ya uongo ikionyesha Simba wanalipa mkopo wa dola za Kimarekani 300,000, takriban Sh. Milioni 700.

Katika shitaka la utakatishaji fedha linalomkabili Aveva, imedaiwa Machi 15, 2016 katika benki ya Baclays Mikocheni, Dar es Salaam alijipatia dola za Kimarekani 187,817, takriban Sh. Milioni 400 kutoka wakati akijua zimetokana na zao la kosa la kughushi.

Katika shitaka la sita, imedaiwa Nyange alimsaidia Aveva kujipapatia dola za Kimarekani 187,817, takriban Sh. Milioni 400 kutoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushi

Katika shitaka la saba la kughushi, linaloqakabili mstakiwa wa Aveva, Nyange na Poppe imedaiwa katika tarehe hizo hizo kwa pomoja walighushi hati ya malipo ya kibiashara ya Mei 28/ 2016 wakionyesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zinathamani ya dola 40,577, zaidi ya Sh. Milioni 90huku wakijua kwamba sio kweli.

Katika shitaka la nane imedaiwa Aveva aliwasilisha hati ya madai (commercial invoice), ya uongo kwa Levison Kasulwa ya Mei 28/ 2016 kwa madhumuni ya kuonyesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya USD 40,577
Katika shitaka la tisa, Aveva, Nyange na Hans Poppe kati ya Machi 10 na Septemba 30, mwaka 2016 waliwasilisha nyaraka za uongo kuonyesha Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya dola za Kimarekani 40,577.

Katika shtaka la mwisho imedaiwa, kati ya Machi na Septemba 2016 Lauwo aliendesha biashara kama mkandarasi kwa kujenga uwanja wa Simba uliopo Bunju wakati akiwa hajasajiliwa

Hata hivyo washtakiwa wamekana mashtaka hayo yote na wamepelekwa rumande kwa sababu shtaka la utakatishaji fedha linalowakabili halina dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 14, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na kufuatilia kama washitakiwa hao wawili watakuwa wamekamatwa.

Bin Buzeiry
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’