Tutaongeza wengine dirisha dogo - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2024
Tutaongeza wengine dirisha dogo - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema usajili wa mlinzi wa pembeni Israel Mwenda ni moja ya sajili ambazo zimekamilishwa kwa kuzingatia mapendekezo ya benchi la ufundi

Kamwe amesema ripoti ya benchi la ufundi ambayo iliwasilishwa kwa Mtendaji Mkuu imetoa mapendekezo ya maboresho ambayo yanahitajika katika dirisha hili

Hivyo Yanga inatarajiwa kusajili wachezaji wengine kabla ya dirisha kufungwa Januari 15 2025

"Tumemsajili Mwenda (Israel) kwa mkopo wa miezi sita hadi mwisho wa msimu lakini niwaambie tu Wanachama na Mashabiki wetu tutasajili wachezaji wengine katika nafasi tofauti kwa kuzingatia mapendekezo ya benchi la ufundi"

"Uongozi wa Yanga unafanya kazi kubwa kupata wachezaji sahihi katika maeneo hayo. Changamoto iliyopo ni kuwa wachezaji wengi wana mikataba na wengine ni tegemeo katika timu zao hivyo kupelekea majadiliano kuchukua muda mrefu"

"Lakini niwahakikishie tutakamilisha usajili wetu mapema kabla ya dirisha dogo kufungwa," alisema Kamwe

Mwenda huenda akaanza kuonekana kesho katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc ambao utapigwa uwanja wa KMC Complex

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’