Mkemi awashangaa Simba, Azam TV

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 May 2018
Mkemi awashangaa Simba, Azam TV
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga Salum Mkemi ameshangazwa na kitendo cha televisheni ya Azam kutolitilia kabisa mkazo tukio la Kelvin Yondani kutemewa mate na Shafiq Batambuze kwenye mchezo kati ya Singida United dhidi ya Yanga badala yake kulianika zaidi tukio la Yondani kumtemea mate Kwasi juzi.

Tukio la Yondani kutemewa mate halikuripotiwa kabisa na vyombo vya habari pengine kwa sababu halikuchukuliwa na kamera za Azam TV, lakini kamera hizo hizo zilimuonyesha Yondani akimlalamikia mwamuzi kuwa ametemewa mate kama alivyofanya Kwasi juzi.

Kumekuwa na presha kubwa hasa kutoka klabu ya Simba kupitia msemaji wao Haji Manara ambaye 'anaishinikiza' Kamati ya saa 72 ya TFF imfungie Yondani baada ya tukio la kumtemea mate Kwasi.

Mkemi amesema Yanga haiungi mkono vitendo visivyo vya kiungwana katika soka lakini ni muhimu haki itendeke sawa kwa kila mchezaji anayefanya kosa lile lile na isiwe makosa yawe yanaonekana yakiwa yamefanywa na wachezaji wa Yanga tu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’