Yanga iko katika hatua za mwisho kuwaongezea mikataba nyota wake raia wa Ivory Coast Pacome Zouazoua na Yao Kouassi, imefahamika
Pacome na Yao walitua Yanga msimu uliopita wakitokea Asec Mimosas kila mmoja akisaini mkataba wa miaka miwili
Mikataba yao iliyosalia ni chini ya miezi sita lakini habari njema ni kuwa mazungumzo ya kuwaongeza mikataba yamekamilika kwa mafanikio na kinachosubiriwa ni nyota hao kumwaga wino
Yanga inaendelea na utaratibu wa kuwabakisha wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza hasa ikizingatiwa bado malengo makubwa ya kutwaa ubingwa Afrika hayajakamilika
Msimu huu Yanga ilifanikiwa kuwaongeza mikataba Djigui Diarra na Stephane Aziz Ki ambao licha ya kupokea ofa nyingi, wakachagua kubaki katika project Yanga
ADVERTISE HERE