Mlinda lango namba moja wa Yanga Djigui Diarra anaweza kukosa mechi zote tatu za ligi kuu zilizobaki kukamilisha duru ya kwanza kutokana na majeraha
Diarra aliumia katika mchezo dhidi ya TP Mazembe na alikosa mchezo dhidi ya Mashujaa Fc langoni akikaa Aboubakar Khomein
Diarra anaweza kukaa nje hadi wiki tatu na pengine anaweza pia kukosa mechi ya marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe itakayopigwa Januari 03, 2024
Katika kipindi hiki Yanga itawategemea walinda lango wake wawili waliobaki Khomein na Aboutwalib Mshery

Mshery bado hajadaka mchezo wowote kwenye ligi msimu huu lakini haitashangaza kama akikaa langoni katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons hapo kesho
Khomein amekuwa na nyakati nzuri katika mechi alizodaka msimu huu lakini unaweza kusema hakuwa na siku nzuri katika mchezo dhidi ya Mashujaa Fc akiruhusu mabao mawili ya mashuti ya mbali