Dodoma Jiji jana hawakukiepuka kikombe cha Wananchi wakibamizwa mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri
Aina mpya ya uchezaji iliyoletwa na kocha Sead Ramovic imeanza kuwasumbua wengi, ni suala la muda tu ile milio ya kumlaumu GSM itaanza kusikika tena
Unaweza kusema Dodoma Jiji jana 'walinyimwa pumzi' na Wananchi, 'pressing' ya Yanga ikiongozwa na Stephane Aziz Ki, Dube, Clement Mzize na Pacome iliwapa wakati mgumu Dodoma Jiji kucheza kuanzia golini kwao
Mabao mawili kati ya manne yaliyofungwa yalikuwa ni matokeo ya Yanga kunyan'ganya mipira eneo la Dodoma Jiji
Wachezaji wa Yanga 'fitness' yao inaonekana kuimarika kwani wamekuwa wakikimbia eneo kubwa la uwanja
Wakati alipotua Yanga, Ramovic aliweka bayana kuwa anapenda timu yake icheze soka la kasi na kuwapa wakati mgumu wapinzani pale wanapokuwa na mpira
Chini ya Ramovic Yanga imeshinda mechi zote nne za Ligi Kuu na kipigo kimekuwa kikiongezea siku hadi siku
Alianza na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Namungo Fc, ukafuata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Mashujaa Fc, ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons, dozi hiyo ikarudiwa jana dhidi ya Dodoma Jiji