Jumapili Januari 12 Yanga itakuwa dimbani Mauritania kumenyana na Al Hilal katika mchezo wa raundi ya tano hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika
Ni mechi muhimu kwa Yanga kusaka ushindi ili kuweka hai matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali. Dakika 180 za mechi mbili zilizobaki, zina umuhimu wa kipekee kwa Yanga
Alama sita zitaihakikishia Yanga kufuzu robo fainali moja kwa moja, ikishindikana alama nne pia zinaweza kuipa nafasi Yanga
Yanga haipaswi kupoteza mchezo dhidi ya Al Hilal, pia ni LAZIMA kushinda mchezo dhidi ya MC Alger
Kama Yanga itashinda dhidi ya Al Hilal basi itahitaji ushindi wa aina yoyote dhidi ya MC Alger (au sare) ili kufuzu kutegemea na matokeo ya mchezo kati ya MC Alger dhidi ya TP Mazembe
Lakini kama Yanga itatoka sare dhidi ya Al Hilal, itahitaji ushindi wa kuanzia mabao 3-0 dhidi ya MC Alger ili kufuzu robo fainali
Kama ilivyokuwa msimu uliopita, Yanga inaweza kukata tiketi ya kwenda robo fainali dimba la Mkapa Januari 19 lakini kwanza inapaswa kuhakikisha haipotezi mchezo unaofuata dhidi ya Al Hilal