Mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda ameweka malengo ya kuhakikisha anafunga mabao mengi msimu huu ili kuisaidia Yanga kufikia matarajio yake
Musonda amerejea kikosini baada ya kupona majeraha ya kidole cha mguu yaliyomuweka nje kwa wiki kadhaa
Nyota huyo kutoka Zambia amekiri kuwa hajafikia malengo yake katika kupachika mabao tofauti na anapokuwa katika timu ya Taifa akitaja sababu ni kutokana na majukumu anayopewa awapo uwanjani
"Nilipokuja hapa nilikuta mshambuliaji mwingine (Mayele) akicheza nafasi ya ushambuliaji wa kati , hivyo nikajitolea kucheza winga. Lakini jukumu langu ni tofauti ninapokuwa mshambuliaji wa kati"
"Hii ndiyo sababu watu hujiuliza kwa nini ninafunga zaidi nikiwa timu ya taifa, ni kwa sababu ninacheza kama mshambuliaji halisi"
"Nililetwa hapa kama mshambuliaji, jukumu langu ni kufunga mabao na kusaidia timu kushinda. Hata hivyo, lazima kwanza nithibitishe uwezo wangu kwa kocha mpya ili nipate nafasi ya kucheza mara kwa mara," alisema Musonda
Msimu huu Musonda amepachika mabao mawili katika ligi kuu ya NBC lakini ameifungia Zambia mabao 4 katika mechi za kuwania kufuzu Afcon 2025 akiwa mmoja wa wachezaji waliofunga mabao mengi na kuisaidia Zambia kufuzu