Wachezaji Yanga 'kuvuna mamilioni' wakifuzu robo fainali CAF CL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2025
Wachezaji Yanga 'kuvuna mamilioni' wakifuzu robo fainali CAF CL

Malengo ya Yanga kwa sasa ni kushinda mechi mbili zijazo za Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Hilal (ugenini) na MC Alger (nyumbani) ili wafuzu robo fainali ya michuano hiyo.

Yanga inapiga hesabu hizo bila ya kuangalia MC Alger na TP Mazembe watafanya nini katika mechi zao kwani ndiyo timu zinazowania nafasi moja ya kufuzu robo fainali kutoka Kundi A baada ya Al Hilal kutangulia.

Kutokana na hilo, ni kwamba bosi wa klabu hiyo, Gharib Said Mohamed (GSM) kawaahidi mastaa wa kikosi hicho kiasi cha shilingi milioni 500 kama wataichapa Al Hilal na MC Alger.

Ahadi hiyo ilitolewa baada ya Yanga kuichapa TP Mazembe mabao 3-1 katika mchezo uliopita uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kufufua zaidi ya kufuzu robo fainali kutokana na kufikisha alama nne. Vinara Al Hilal waliotangulia robo fainali wana alama 10, MC Alger (5) na TP Mazembe (2) wakiburuza mkia.

Taarifa za ndani zimedokeza kuwa, mastaa wa Yanga wamewekewa ahadi hiyo endapo wakishinda mechi hizo mbili zilizobaki na kutinga robo fainali ambapo itakuwa ni mara ya pili mfululizo kufanya hivyo baada ya msimu uliopita walipokuwa wakifundishwa na Miguel Gamondi.

"Bosi mwenyewe (GSM) ndiye amewaahidi kiasi hicho cha fedha shilingi milioni 500 kama bonasi yao, hivyo lazima wapambane ili kuvuna alama sita ugenini na nyumbani," kilisema chanzo hicho

Ni wazi kuwa, mastaa wa Yanga watahitaji kupambana katika mechi hizo wakianza dhidi ya Al Hilal ili kushinda mchezo huo. Mchezo wa kwanza Yanga ilikutana na kipigo cha mabao 2-0 nyumbani.

Jumapili ya wiki hii Yanga itakuwa ugenini kukabiliana na Al Hilal katika mchezo unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa Cheikha Ould Boadiya uliopo Nouakchott nchini Mauritania kuanzia saa 4:00 usiku.

Baada ya hapo, Yanga itarejea nyumbani kumalizana na MC Alger kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Januari 18 ukiwa ni mchezo wa mwisho wa Kundi A

Kabla ya Yanga haijacheza dhidi ya Al Hilal, kule Algeria wenyeji MC Alger watawakaribisha TP Mazembe, mechi ikichezwa Ijumaa wiki hii. TP Mazembe itamalizia nyumbani dhidi ya Al Hilal siku moja ambayo pia Yanga itakuwa ikicheza na MC Alger. Baada ya hapo, itafahamika nani ataungana na Al Hilal kufuzu robo fainali kutoka Kundi A

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’