Imeelezwa klabu ya Wydad Athletic imetuma ofa Jangwani kwa mara nyingine kuwataka wachezaji Clement Mzize na Stephane Aziz Ki
Hata hivyo Yanga imeendelea na msimamo wake katika dau la usajili ambapo thamani ya kila mchezaji sio chini ya Tsh Bilioni 2
Wydad wameelekezwa kama wako tayari, itawalazimu kusubiri hadi mwisho wa msimu kwa kuwa kwa sasa Yanga haiko tayari kuwaachia hasa ikizingatiwa ina malengo ya kufanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa na kutetea mataji yote ya ndani
Mzize ameendelea kuzivutia timu nyingi, miezi michache iliyopita, mkufunzi wa Kaizer Chiefs Nasreddine Nabi alikuja nchini kufanya mazungumzo na uongozi wa Yanga juu ya mchezaji huyo
Hata hivyo hakukuwa na mwafaka uliofikiwa lakini Chiefs wanaonekana bado hawajakata tamaa na huenda wakarudi tena Jangwani mwishoni mwa msimu
Kwa kiwango ambacho Mzize ameendelea kukionyesha, lolote linaweza kutokea pale msimu utakapomalizika