Ramovic amewafunga midomo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Jan 2025
Ramovic amewafunga midomo

Alipopoteza mechi mbili za awali hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa, wengi walimaliza maneno na baadhi hata kufika mbali kwa kumlaumu Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kwa kumuajiri kocha Sead Ramovic wakidai hana 'CV' ya kuifundisha Yanga kwani timu aliyotoka Afrika Kusini ilikuwa ikiburuza mkia

Wengi ambao 'walimaliza maneno' wakati ule hutawasikia wakizungumza sasa kwani Ramovic amewaziba midomo

Ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Hilal jana ulikuwa mfululizo wa kiwango bora cha kikosi cha Yanga kilichoimarika baada ya wiki tano za mazoezi makali chini ya Ramovic

Ulikuwa ushindi wa sita mfululizo kwa Yanga ambayo sasa inahitaji alama tatu tu katika mchezo unaofuata kwenye ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger ili kufuzu robo fainali

Yanga haijapoteza mchezo katika mechi 7 zilizopita, ikishinda mechi 6 mfululizo na kutoka sare mchezo mmoja. Imefunga mabao 21 huku ikiruhusu mabao manne tu

Gusa achia twende kwao imekolea na kinachofuta sasa ni vipigo kwa kila atakayekatiza mbele..!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’