Wananchi wameendelea kununua tiketi kwa wingi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya MC Alger ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Hadi kufikia Ijumaa jioni, tiketi za VIP A zimemalizika huku tiketi chache za VIP B zikielekea ukingoni
Tiketi za VIP C nazo zimebaki chache huku karibu asilimia 60 za tiketi za Mzunguuko pia zimeshauzwa
Mkakati wa Yanga ni kuhakikisha mashabiki 60,000 wanaingia dimba la Mkapa hapo kesho kuongeza hamasa katika mchezo dhidi ya MC Alger utakaopigwa saa 10 jioni
ADVERTISE HERE