Tutafanya maboresho tuwe bora zaidi - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2025
Tutafanya maboresho tuwe bora zaidi - Kamwe

Klabu ya Yanga imesema ilifanya kila kitu kuanzia kwenye uongozi, benchi la ufundi na wachezaji kuhakikisha wanafuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini haikuwa riziki yao kwa msimu huu

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa mabingwa hao wa Tanzania Bara, Ali Kamwe, aliwataka wanachama na mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu na wavumilivu kwa wanachopitia hivi sasa, kwani wanajipanga kwa ajili ya msimu ujao warudi na nguvu mpya, ikiwamo kufanya maboresho ya usajili kwenye dirisha kubwa

"Haikuwa riziki. Hicho ndicho nachoweza kusema. Tumshukuru Mungu kwa sababu watu wote waliokwenda uwanjani, walikwenda kuona Yanga ikifuzu robo fainali, kilichotokea kila mtu ameona, si riziki, tutajipanga wakati ujao, nadhani tutafanya maboresho msimu ujao, kila ambacho tunaweza kufanya kilifanyika ili tufuzu jamaa walikuwa vizuri sana," alisema Kamwe

Kamwe Amesema kwa sasa kumekuwa na maoni mengi kutoka kwa wanachama, mashabiki na wadau wa soka kuhusu nini kilikosewa na nini kifanyike, akisema mawazo yote yamekusanywa na wanayafanyiwa kazi

"Unapokuwa kiongozi unakusanya kila kitu, kwa wanaosema hatukujipanga vizuri sawa, wanaotushauri tumekusanya ushauri wao na tunaufanyia kazi, ila kwa sasa kazi tuliokuwa nayo ni kukusanya makombe yetu, la Ligi Kuu na Kombe la FA, ili msimu ujao turudi tena kwa ngumu kubwa," alisema

Yanga imewashukuru wanachama na mashabiki wote waliowaunga mkono kwa njia moja ama nyingine kufika hapo walipofika, pamoja na wale waliokuwa wakifika uwanjani, hususan kwenye mchezo wa mwisho Jumamosi iliyopita

"Shukrani kwa wanachama na mashabiki wote wa Yanga waliofika Uwanja wa Mkapa, Jumamosi iliyopita. Uwapo wenu na sauti zenu zilikuwa na thamani kubwa sana. Kumepambazuka, ni siku mpya, ya jana yameshapita yatupasa kusahau. Kila huzuni tuliyonayo moyoni, tuigeuze kuwa hamasa ya kutupa morali ya kuupambania ubingwa wetu wa Ligi Kuu na Kombe la FA"

"Tuko katikati ya mapambano, yatupasa kujidhatiti kweli kweli kurudisha makombe yetu kabatini na hili ni muhimu kuliko vyote. Tusongeni mbele kama kaulimbiu inavyosema, daima mbele nyuma mwiko," alihitimisha Kamwe

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’