Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amealikwa na Shirikisho la soka la Africa CAF kuhudhuria hafla ya droo ya AFCON 2025 itakayofanyika Jumanne ijayo nchini Morocco
Kamwe anakuwa msemaji wa kwanza wa klabu ya Tanzania kualikwa katika hafla kubwa ya CAF
Wanasema unapofanya kazi nzuri inaonekana, mwaliko huu ni kuonyesha CAF wametambua kile ambacho Kamwe anafanya ndani ya Yanga
Kamwe amesema mwaliko huo unakwenda sambamba na majukumu ya kulitangaza tukio lenyewe kwani yeye ni sehemu ya kitengo ya 'promo' kilichoundwa CAF
"Nitaondoka Tanzania tarehe 24 kuelekea Morocco kuhudhuria tukio la droo ya makundi ya Afcon 2025. Nitakuwa Morocco kwa muda wa wiki nzima kwani pia nitakuwa na jukumu la kufanya 'promo' ya tukio lenyewe," alisema Kamwe