Ikangalombo, Mwenda tayari kwa mechi ya kwanza Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jan 2025
Ikangalombo, Mwenda tayari kwa mechi ya kwanza Yanga

Jumamosi, Januari 25 Yanga inaanza kampeni ya kutetea kombe la Shirikisho la CRDB kwa kumenyana na Copco Fc katika mchezo wa raundi ya pili utakaopigwa uwanja wa KMC Complex

Yanga ilirejea mazoezini jana kujiandaa na mchezo huo ambapo huenda kocha Sead Ramovic akatumia kikosi tofauti na kile kilichozoeleka akiwapa mapumziko wachezaji waliotumika zaidi

Lakini pia itakuwa nafasi kwa mashabiki wa Yanga kuwashuhudia nyota wapya waliosajiliwa dirisha dogo Israel Mwenda na Jonathan Ikangalombo

Tangu usajili wao ukamilike, Mwenda na Ikangalombo bado hawajaonekana katika mechi rasmi ya Yanga

Licha ya kusajili kutumika katika ligi ya mabingwa, Mwenda hakupata nafasi katika mchezo dhidi ya MC Alger ambao ulikuwa mchezo wa mwisho kwa Yanga katika michuano hiyo msimu huu kwani Wananchi waliaga mashindano baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana

Ikangalombo hakuwa na sifa ya kuichezea Yanga katika mashindano ya CAF msimu huu kwani tayari alikuwa ameitumikia AS Vita katika hatua za awali

Bila shaka Ikangalombo yuko tayari kuonyesha thamani yake na kudhihirisha ubora baada ya usajili wake kuzungumzzwa zaidi katika dirisha dogo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’