Baada ya kutemwa na Yanga, mshambuliaji Mcongomani Jean Baleke, anakaribia kujiunga na Amazulu inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini, imefahamika
Yanga iliachana na Baleke kwenye dirisha dogo nafasi yake ikichukuliwa na Mcongomani mwenzake winga Jonathan Ikangalombo aliyetua kutoka AS Vita ya DR Congo
Baleke alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu akitokea klabu ya TP Mazembe kwa mkopo
Hata hivyo alishindwa kulishawishi benchi la ufundi la Yanga na hivyo uongozi kuamua kumrejesha katika timu yake, TP Mazembe
Baleke aliifungia Yanga bao moja tu katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union uliopigwa dimba la Sheikh Amri Abeid
ADVERTISE HERE