Baada ya kukosekana katika kikosi cha Yanga kwa takribani wiki nne akiwa majeruhi, kiungo mshambuliaji Maxi Nzengeli jana alirejea dimbani akiingia kipindi cha pili katika mchezo wa raundi ya pili kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Copco Fc
Katika mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0, Maxi alifunga moja ya mabao hayo kupitia mkwaju wa penati akifunga kupitia staili ya panenka
Kilichowapa furaha zaidi mashabiki wa Yanga ni kumshuhudia Maxi akiwa fit na kuisaidia Yanga kushinda mchezo huo ambao mpaka mapumziko Wananchi walikuwa wamefunga bao moja tu
Maxi amekuwa mchezaji muhimu tangu alipotua kwa Wananchi msimu uliopita akitokea Maniema Union ya DR Congo
Kurejea kwake sasa kunampa mtihani kocha Sead Ramovic ambaye pengine atalazimika kupangua kikosi chake cha kwanza
Ikumbukwe pia Yanga imeongeza wingi mwingine Jonathan Ikangalombo ambaye hata hivyo jana hakucheza kocha Ramovic akimpa program maalum ya mazoezi ambayo anapaswa kuikamilisha kabla ya kuanza kucheza