Mkwasa ataja sababu ya baadhi ya wachezaji kutosafiri Algeria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 May 2018
Mkwasa ataja sababu ya baadhi ya wachezaji kutosafiri Algeria
Uongozi wa Yanga umewakingia kifua wachezaji wake Kelvin Yondani 'Vidic', Ibrahim Ajib, Papy Tshishimbi na Mzambia Obrey Chirwa walishindwa kusafiri na timu kwenda nchini Algeria kwa sababu ya matatizo mbalimbali.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa amesema, wachezaji hao hawajasafiri si kukusudia, lakini kwa sababu ya matatizo mbalimbali.

Mkwasa amesema, Yondani na Tshishimbi wao walipata maumivu katika mchezo uliopita dhidi ya Simba, Obrey ana malaria wakati Ajib anamwangalia mke wake anayetarajiwa kujifungua hivi karibuni.

"Kama nilivyosema, Yondani, Tshishimbi na Chirwa wao ni wagonjwa na Ajib amebaki kwa sababu mkewe anakaribia kujifungua,"amesema Mkwasa.

Kikosi cha Yanga kilisafiri na Ndege ya Emirates jana Alhamisi kwenda Algeria wakipitia Dubai tayari kwa mchezo huo utakaochezwa keshokutwa Jumapili dhidi ya USM Alger.

Wachezaji wa Yanga waliondoka na timu ni Rostand Youthe, Ramadhan Kabwili, Hassan Kessy, Andrew Vincent, Haji Mwinyi, Gadiel Michael, Pato Ngonyani, Said Makapu, Juma Abdul, Yussuf Mhilu, Mwashiuya Geoffrey, Pius Buswita, Rafael Daud, Yohana Nkomola, Emmanuel Martin, Juma Mahadhi, Abdallah Shaibu 'Ninja', na Said Makapu.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’