Mchezaji kiraka Israel Mwenda jana aliitumikia Yanga kwa mara ya kwanza katika mchezo wa raundi ya pili kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Copco Fc uliopigwa uwanja wa KMC Complex
Mwenda 'alizima' dakika zote 90 za mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-0 akihusika katika mabao mawili ambayo alitoa 'assist'
Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic alimuanzisha safu ya ulinzi upande wa kulia katika kipindi cha kwanza lakini baada ya mapumziko akambadilishia majukumu na kumpeleka winga ya kulia huku Kibwana Shomari akiingia kucheza namba 2
Ushirikiano wake na Kibwana upande wa kulia ni kitu kilichowavutia wengi ambapo wawili hao walikuwa wakibadilishana majukumu ya winga na beki
Mwenda alionekana kuwa mahiri zaidi katika upigaji wa krosi eneo ambalo huenda likambeba zaidi katika kikosi cha Ramovic
Mwenda ni mtambo mwingine wa kupika mabao kutokea pembeni...!