Yanga yalegeza msimamo kwa Mzize

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jan 2025
Yanga yalegeza msimamo kwa Mzize

Baada ya kupokea ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali, klabu ya Yanga imelegeza msimamo na sasa huenda ikamuuza mshambuliaji Clement Mzize katika dirisha lijalo la usajili, imefahamika

Wakati klabu nne za Uarabuni zikisubiri majibu ya Yanga juu ya utayari wao wakiwa tayari wameshaweka fedha ndefu mezani, taarifa mpya ni kwamba kuna klabu nyingine ya Ulaya nayo imepiga hodi ikimtaka mshambuliaji huyo.

Ukiacha ofa za klabu hizo kutoka Afrika Kaskazini zinazofikia Sh2 Bilioni, klabu hiyo ya Ubelgiji inataka kutoa zaidi ya fedha hizo kufikia 2.5 bilioni.

Mmoja wa maafisa waandamizi wa Yanga amedokeza uwezekano wa Mzize kuuzwa baada ya klabu kuvutiwa dau hilo lakini muhimu zaidi ni kuzingatia maslahi ya mchezaji

"Tunafikiria kufanya biashara fedha zinazosemwa ni nyingi unajua pia tunataka kufikiria juu ya maisha ya baadaye ya mchezaji ili akajiendeleze tutaangalia ofa ipi itakuwa sahihi zaidi kwa klabu na kwake," Afisa huyo alinukuliwa na Mwanaspoti

Msimu huu Mzize yuko 'on-fire' akifunga mabao 12 katika mashindano yote pia akitoa assist nne

Amefunga mabao 5 katika ligi ya mabingwa kuanzia hatua ya awali huku akifunga mabao 6 katika ligi kuu, bao 1 akifunga kwenye Ngao ya Jamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’