Kesho Jumamosi, Februari 1 mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inarejea baada ya mapumziko ya mwezi mzima
Mabingwa watetezi Yanga wanarejea na mechi ya kiporo dhidi ya Kagera Sugar. Mchezo huo utapigwa uwanja wa KMC Complex saa 10 jioni
Yanga itashuka dimba la KMC Complex ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 timu hizo zilipokutana kwenye duru ya kwanza
Katika misimu ya karibuni takwimu zinaonyesha Yanga imepata matokeo mazuri mbele ya wapinzani wao hao ambapo katika mechi tano zilizopita Yanga imeshinda nne na moja ni sare
Kagera Sugar haikufunga bao lolote katika mechi hizo ambazo Wananchi waliondoka na 'cleansheet'
Ushindi kwa Yanga utawahakikishia Wananchi kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi wakati Kagera Sugar wanaoshika nafasi ya 15 wanazihitaji alama 3 ili wajiondoe katika eneo la hatari la kushuka daraja
Kikosi cha kocha Sead Ramovic kimeifunga kila timu kwenye ligi katika mechi tano zilizopita tangu Mjerumani huyo akipokabidhiwa mikoba iliyoachwa na Miguel Gamondi
Ni wazi Kagera Sugar watahitaji kuwa katika ubora mkubwa ili kuizuia Gusa Achia Twende Kwao ya Ramovic ambayo imesababisha Yanga kufunga mabao 23 katika mechi 6 zilizopita kwenye ligi na FA