Gusa Achia Twende Kwao inakolea

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Feb 2025
Gusa Achia Twende Kwao inakolea

Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema mwenendo wa kikosi chake unampa matumaini kuwa watafikia malengo ya kuwa na timu bora na yenye ushindani zaidi

Tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa Yanga, Ramovic amewaongoza Wananchi kushinda mechi zote sita za ligi kuu wakifunga mabao 22 na kuruhusu mabao mawili tu

Akizungumza baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Kagera Sugar juzi, Ramovic alisema sasa wanatengeneza nafasi nyingi na kuzitumia ingawa sio kwa ufanisi mkubwa

Lakini pia timu imeendelea kuwa imara katika kujilinda ambapo amesema wachezaji wote wanatimiza vyema majukumu yao pale wanapokuwa hawana mpira

"Nafurahi kuona wachezaji wanaimarika kadiri ya siku zinavyosogea, kasi, nguvu na juhudi uwanjani inazidi kuwa kubwa kwa kiwango kinachovutia, tunafunga mabao lakini najua hatuwezi kutumia kila nafasi ila tunaweza kufunga mabao zaidi"

"Ukitazama kama tuna safu ya ulinzi nzuri ni sawa mabeki wanafanya vizuri lakini hapa ningependa kuiangalia timu nzima namna tunavyopoteza mpira wote tunapambana kuuondoa kwenye umiliki wa wapinzani na hili limekuwa likifanyika vizuri"

"Nawapongeza wachezaji wamecheza vizuri pamoja na kukutana na timu ambayo ilikuwa na mpango wa kujilinda zaidi na kutumia mipira ya kushtukiza wameweza kuwapita na kufunga mabao zaidi ya matatu," alisema Ramovic

Katika mechi zake 6, Ramovic ameivunja rekodi ya mabao ya mtangulizi wake Miguel Gamondi ambaye katika mechi 10 alizokiongoza kikosi cha Yanga msimu huu, timu ilifunga mabao 12 tu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’