Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amesema ameendelea kukiimarisha kikosi chake hasa katika eneo la mwisho ili kuhakikisha wanatumia vyema nafasi wanazotengeneza
Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo dhidi ya KenGold utakaopigwa kesho Jumatano katika uwanja wa KMC Complex, Ramovic alisema ni jambo jema kwa timu yake kufunga mabao mengi katika kila mechi lakini wanahitaji kuongeza ufanisi katika eneo la umaliziaji
"Nafurahi tumekuwa tukishinda na kufunga mabao mengi, hilo ni jambo jema kwetu lakin nafikiri tunaweza kufunga zaidi kama tutatumia vyema nafasi nyingi tunazotengeneza"
"Hivyo tumejiandaa vyema kwa mchezo dhidi ya KenGold, tumefanyia kazi baadhi ya changamoto ili kuhakikisha tunashinda mchezo huo"
"Tunatarajia mchezo dhidi ya KenGold utakuwa mgumu kwani nafahamu timu hii imefanya maboresho makubwa"
"Sitarajii mabadiliko ya kiuchezaji kama zilivyofanya timu nyingine, watakuwa wengi katika kujilinda hivyo tutahitaji kuwafungua ili kupata mianya ya kupitisha mipira na kufunga mabao"
"Yanga ni timu bora Tanzania, tumetwaa ubingwa kwa misimu mitatu mfululizo, tunahitaji kushinda mchezo huu kwani lengo letu ni kutetea taji letu," alisema Ramovic