Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Sead Ramovic amewaaga mashabiki na wanachama wa timu hiyo baada ya makubaliano ya pande mbili ya kusitisha mkataba wake kufikiwa
Ramovic amejiunga na klabu ya CR Belouizdad ya Algeria akitarajiwa kutangazwa wakati wowote kuwa kocha mkuu wa timu hiyo
Kocha huyo raia wa Ujerumani amemshukuru Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kwa kumuamini na kumpatia nafasi ya kuwanoa mabingwa hao wa nchi
"Ninatoa shukrani zangu za dhati kwa Rais (Injinia Hersi Said) kwa imani na fursa nzuri ya kuwa sehemu ya klabu hii kubwa"
"Maono yake na uongozi wake umefanya safari yangu hapa kuwa ya pekee sana, na nitaendelea kushukuru kwa hilo"
"Kwa wachezaji, wafanyakazi, na mashabiki, asante kwa shauku, kujitolea na imani yenu. Muda wangu katika Young Africans umekuwa mojawapo ya matukio mazuri na yenye kufurahisha maishani mwangu"
"Klabu hii ina mustakabali mzuri, na sina shaka kuwa itaendelea kupata mambo makubwa. Endeleeni kupambana, endeleeni kuamini, na endeleeni kuweka historia"
"Asante sana, na kila la kheri!," aliandika Ramovic katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii