Kwenye makala iliyopita tulizungumza kuhusu mkakati wa timu ile inavyowatumia marefa kushinda mechi zao
Katika mechi yao liyopita kilipigwa kwa dakika 103, pengine ni rekodi msimu huu mechi kupigwa kwa dakika 13 zaidi baada ya 90 kumalizika
Ziliongezwa dakika 9 lakini baada ya muda huo kuisha na 'hakijaeleweka', 'bwana mwamuzi' akaongeza zake nne lakini Mungu alikuwa upande wa wapinzani
Utata pia uligubika aina ya goli walilofunga timu ile na kama haitoshi 'bwana mwamuzi' akafanya kituko cha mwaka kwa kumuonyesha mlinda lango wa wapinzani kadi ya njano na nyekundu kwa wakati mmoja huku akioneka kutoa kadi hizo akiwa na jazba!
Wakati huo wapinzani walikuwa wamemaliza 'sub' zao na hivyo mchezaji wa ndani kulazimika kukaa langoni kumalizia dakika zilizokuwa zimebaki
Unaweza kusema mkeka ulichanika jana, haikuwezekana kuhalalisha 'HARAMU..!'