Jana mshambuliaji chipukizi wa Yanga Yohana Nkomola alilazimika kukimbizwa Hospitalini baada ya kuugua ghafla muda mfupi tu Yanga ilipowasili nchini Algeria.
Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu amethibitisha Nkomola kukumbwa na mkasa huo lakini amesema tayari amepatiwa matibabu na anaendelea vizuri.
"Ni kweli Nkomola alipata maradhi ambayo yamesababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa. Tayari ametibiwa na anaweza kucheza mchezo wa kesho dhidi ya USM Alger."
Yanga imesafiri na wachezaji 18 pekee na inahitaji utimamu wa afya wa kila mmoja kuelekea mchezo huo utakaopigwa saa nne usiku wa saa za Tanzania

ADVERTISE HERE