Jumatatu, Februari 10 Kocha Mpya wa Yanga Miloud Hamdi anatarajiwa kuanza rasmi majukumu yake kwa kukiongoza kikosi chake katika mchezo wa kwanza wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Meja Jenerali Isaamuhyo, mbweni jijini Dar es salaam
Wakati Yanga ikimenyana na KenGold juzi, Hamdi alikuwa jukwaani kushuhudia mchezo huo ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 6-1, matokeo ambayo yalitosha kuwarejesha kileleni mwa msimamo wa ligi
Hamdi atakuwa na mechi 13 za kuhakikisha Yanga haitoki kileleni ili kukamilisha lengo la kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo
Kudhihirisha yuko tayari kwa majukumu yake mapya, akiwa jukwaani juzi, Hamdi alionekana akichukua 'notisi' katika kitabu chake kidogo pamoja na kutoa maelekezo mbalimbali
Wale waliodhani Yanga itapungua makali baada ya Ramovic kuondoka waandike maumivu, kwani Hamdi anaweza kuwasababishia vilio vikubwa zaidi
Alikaribishwa kwa ushindi wa mabao sita, yeye sasa ataanzia hapo...!