Mlinzi wa kati wa Yanga Dickson Job ni miongoni mwa wachezaji ambao mikataba yao inaelekea ukingoni mwisho wa msimu lakini uhakika ni kuwa Job haendi popote
Yanga tayari imeanza michakato ya kuwaongezea mikataba wachezaji wake ambao mikataba yao inafika tamati mwishoni mwa msimu na bado wanahitajika kikosini
Job ameitumikia Yanga kwa misimu minne akitua mwaka 2021 akitokea klabu ya Mtibwa Sugar kwenye usajili wa dirisha dogo
Usajili wake lilikuwa pendekezo la Cedrick Kaze ambaye wakati huo alikuwa kocha mkuu wa Yanga. Baadae aliondoka na kurejea tena akiwa kocha msaidizi
Job ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha Yanga na timu ya Taifa akiwa ni nahodha msaidizi
Bila shaka Job ataendelea kuwahudumia Wananchi labda itokee apate ofa kubwa zaidi kutoka nje ya nchi kwani licha ya ofa zinazomiminika kwake, mwenyewe kipaumbele chake ni Yanga kutokana na namna alivyoaminiwa na kupewa nafasi ya kucheza tangu amejiunga nayo