Yanga yatimiza miaka 90

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Feb 2025
Yanga yatimiza miaka 90

Tarehe kama ya leo 11/02/1935 klabu ya Yanga ilianzishwa rasmi, imetimiza miaka 90 toka kuanzishwa kwake

Katika kuadhimisha miaka 90 ya mabingwa hao wa historia Yanga, Februari 11 uongozi wa Yanga uliandaa matukio mbalimbali ambayo yalifanyika yakishirikisha wachezaji, viongoni na wanachama wa Yanga

Ni miaka 90 ya furaha kwa Wananchi, ukizungumzia timu yenye mafanikio zaidi katika ardhi ya Tanzania basi ni Yanga

Ndio mabingwa mtetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakitwaa taji hilo mara nyingi zaidi (30) pia wakiwa mabingwa wa taji la FA mara nne, wakiwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo pia

Yanga pia wanakishikilia rekodi ya kucheza michezo mingi zaidi bila kufungwa 'unbeaten' ikicheza michezo 49 bila kufungwa msimu wa 2022/23

Mafanikio makubwa wa klabu hiyo kimataifa ni kucheza hatua ya fainali katika Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC 2023) na robo fainali ya ligi ya mabingwa msimu uliopita

Msimu huu haukuwa mzuri sana katika ligi ya mabingwa Yanga ikiondoshwa hatua ya makundi lakini bila shaka ni nafasi ya kujipanga ili kurejea na nguvu kubwa zaidi msimu ujao

Malengo ya Yanga sasa kutetea mataji yote ya ndani yaani Ligi Kuu na FA ambayo wanayashikilia kwa misimu mitatu mfululizo

HAPPY BIRTHDAY YANGA AFRIKA...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’