Unaweza kusema mshambuliaji Jonathan Sowah ambaye alitua Singida Black Stars katika usajili wa dirisha dogo, safari yake kuelekea kwa mabingwa wa nchi Yanga, ni suala la muda tu
Sowah raia wa Ghana jana aliifungia Singida BS bao pekee la ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania uliopigwa uwanja wa Isamuhyo. Hilo lilikuwa bao lake la pili katika mechi tatu alizoitumikia Singida BS
Akizungumza baada ya mchezo huo, Sowah alieleza kufurahi kucheza soka Tanzania akiwasifu Watanzania kwa ukarimu wao kwa wageni lakini zaidi akamtaja Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kama mtu muhimu katika safari yake ya kucheza soka Tanzania
Sowah alisema anaamini muda utafika ataitumikia klabu ya Yanga kwani kuwa katika klabu hiyo ni kama kuwa nyumbani
"Yanga ni nyumbani, hata nilivyopata ofa ya Singida niliwaambia. Rais wa Yanga ni kama baba, najua alichofanya kwangu na kutengeneza maisha yangu"
"Mimi sio mtanzania ila napenda namna watanzania wanavyowapokea watu. Niseme tu, ni jambo la muda ipo siku nitacheza Yanga," alisema Sowah
Taarifa za ndani zimedokeza kuwa Yanga ilishamalizana na Sowah, uongozi ulimpa baraka zote aende akaitumikie Singida BS hadi mwishoni mwa msimu