Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube ameendelea kuwajibu wakosoaji wake kwa vitendo katika ligi kuu ya NBC
Dube jana aliiongoza Yanga kuifumua KMC mabao 6-1 na kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi huku akihusika katika mabao manne
Licha ya kufunga moja ya mabao, Dube alitoa 'hat-trik' ya assist akiendeleza rekodi yake nzuri msimu huu. Amefikisha mabao 8 huku pia akitoa assist 7 katika mechi 19
Dube ndio mchezaji aliyehusika katika mabao mengi zaidi msimu huu. Unaweza kusema kama ligi ingetamatika leo, basi tuzo ya 'MVP' ingekuwa yake
Alianza kwa kusuasua mwanzoni mwa msimu akikumbana na nyakati ngumu na kuwapa mwanya wakosoaji wake 'kumaliza maneno'
Sifa kubwa ya Dube inayomtofautisha na washambuliaji wengine ni uwezo wake wa kushiriki kikamilifu katika mchezo
Haishangazi kuona ndiye mshambuliaji anayeongoza kwa kutoa 'assist' kwani kama hafungi basi anawatengenezea wenzake nafasi
Zipo hoja kuwa anapoteza sana nafasi lakini ni kwa sababu ni mshambuliaji anayejua kutengeneza mazingira ya hizo nafasi kutokea
Ni wazi kama ataongeza ufanisi wake mbele ya lango, tuzo ya mfungaji bora inaweza kwenda kabatini kwake mwishoni mwa msimu