Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki leo anatarajiwa kufunga ndoa na mpenzi wake Hamisa Mobeto baada ya hafla ya kutoa mahari kukamilika hapo jana
Licha ya kukabiliwa na ratiba ya kukamilisha hitaji hilo muhimu katika maisha yake, Aziz Ki ameendelea kufanya mazoezi ya kikosi cha Yanga yakiwa ni maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Singida BS ambao utapigwa kesho Jumatatu dimba la KMC Complex
Hakuna muda wa 'Hooney Moon' kwa sasa kwani Yanga inamuhitaji Aziz Ki katika mkakati wake wa kutetea ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo
Aziz Ki raia wa Burkina Faso leo anaoa na kesho anatarajiwa kuwa uwanjani kuikabili Singida Black Stars
Jumatano, Februari 19 itafanyika sherehe ya harusi na Jumapili Februari 23 Aziz Ki atakuwa mkoani Kigoma kuikabili Mashujaa Fc
