Ukipita huko mitandaoni na kusikiliza uchambuzi katika vipindi vya michezo katika redio mbalimbali utashangazwa na mambo yanayojadiliwa!
Ushindi wa mabao 2-1 ambao Yanga wameupata dhidi ya Singida Black Stars jana ni kama umewaumiza wengi
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alikuwa na kila sababu kusema Yanga ina maadui wengi sana msimu huu ni lazima wafanye kazi ya ziada ili kutetea ubingwa
Yanga sio timu ya kwanza kuifunga Singida BS msimu huu. Kabla ya mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania, Singida Black Stars walicheza dhidi ya KMC katika uwanja huohuo wa KMC Complex na kupoteza mchezo kwa mabao 2-0
KMC alipoifunga Singida BS mabao 2-0 hakukuwa na kauli za Singida BS kuuza mechi lakini walipofungwa mabao 2-1 na Yanga wameuza mechi!
Kumbuka hawa KMC mechi yao iliyopita walifungwa mabao 6-1 na Yanga hapo KMC Complex
Tangu Yanga ianze kutumia uwanja wa KMC Complex, Singida BS ndio timu ya kwanza kufungwa mabao machache, timu nyingine zilifungwa kuanzia mabao matatu wao wamefungwa mawili
Hivyo kwa kiasi kikubwa kocha wa Singida BS alifanikiwa katika mkakati wake wa kimbinu kuidhibiti Yanga
Imefikia hatua baadhi ya wachumbuzi kuhoji kwanini wachezaji flani hawakuanzishwa licha ya kocha wa Singida BS kusema waziwazi alichokifanya ilikuwa mkakati wake katika mchezo huo ambao anaamini alifanikiwa kwa kiasi kikubwa
Inaonekana badhi ya mashabiki na hata wachambuzi walitamani Yanga isipate ushindi dhidi ya Singida BS, ili kuzinufaisha timu zao katika mbio za ubingwa
Lakini wasichojua njia sahihi kwa timu kuwa bingwa ni kushinda mechi zake na sio kutegemea timu nyingine zimfanyie kazi
Misimu yote mitatu mfululizo Yanga imetwaa ubingwa kwa kushinda mechi zake na msimu huu malengo ni hayo
Wale ambao wanataka timu nyingine ziwafanyie kazi ili kuwa mabingwa pengine hawako tayari na hawastahili kuwa mabingwa