Baada ya mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya Singida Black Stars uliomalizika kwa Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dimba la KMC Complex hapo jana, mshambuliaji wa Singida BS Jonathan Sowah akakutana na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said
Sowah ndiye aliyefunga bao pekee la Singida BS likiwa ni bao lake la tatu kwa klabu hiyo aliyojiunga nayo katika usajili wa dirisha dogo
Wiki iliyopita Sowah aliweka wazi ukaribu wake na Injinia Hersi huku akiahidi kuwa ipo siku ataitumikia Yanga
Sowah alibainisha hata ujio wake hapa Tanzania anamshukuru Hersi akisema ni kama baba yake
Ni ndoto ya kila mchezaji kucheza katika timu kubwa. Hapa Tanzania klabu kubwa ni moja tu, Yanga
Bila shaka ndoto ya Sowah kuitumikia Yanga itakamilika, muhimu anapaswa aendee kupambana..