Katika mechi nne zilizopita, mlinda lango namba moja wa Yanga Djigui Diarra ameruhusu mabao matatu
Aliruhusu bao katika mchezo dhidi ya Ken Gold Yanga ikishinda mabao 6-1 uwanja wa KMC Complex
Akaruhusu tena bao katika mchezo dhidi ya KMC Yanga ikiipuka tena na ushindi wa mabao 6-1
Juzi akaruhusu bao la tatu Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars
Mabao aliyoruhusu katika mechi dhidi ya KenGold na Singida BS unaweza kusema ni mabao mepesi ambayo kwa daraja lake hakupaswa kufungwa
Yawezekana ni uchovu ama sababu nyingine ambazo pengine makocha wake katika benchi la ufundi wanaweza kumsaidia
Lakini pia ni makosa ya kibinadamu, ambayo humtokea mchezaji yeyote katika mechi. Diarra amedhihirisha pasipo shaka kuwa yeye ndiye golikipa bora hapa nchini na hata Afrika yuko katika orodha ya makipa watatu bora
Mchezaji yeyote anaweza kufanya makosa, bahati mbaya kwa golikipa makosa yake yanaweza kuigharimu timu hapo hapo yanapofanyika tofauti na mshambuliaji anapokosa nafasi ya wazi au mchezaji mwingine yeyote anapofanya makosa ndani ya uwanja
La muhimu kwa Diarra ni kutambua mafanikio ya Yanga yanategemea ubora wake langoni yeye akiwa kipa namba moja
Katika nyakati hizi ambazo kila mechi ina presha kubwa, Yanga inahitaji ubora na uzoefu wa Diarra ili kuvuka salama