Hamdi azitaka alama tatu Kigoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Feb 2025
Hamdi azitaka alama tatu Kigoma

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema anatarajia mechi dhidi ya Mashujaa Fc itakuwa na upinzani mkali na warahitaji kuwa katika ubora wao kwa dakika zote 90 za mchezo ili kuondoka na alama tatu

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Hamdi amesema Mashujaa Fc ni moja ya timu ngumu katika ligi kuu msimu huu na pengine walistahili kuwa katika nafasi za juu zaidi kuliko hapo walipo

Hata hivyo amesema Yanga ni timu kubwa na hiyo ni sababu wanahitaji kuwa bora katika kila mechi kwani kila timu inatamani kupata ushindi dhidi ya Yanga

"Tunaiheshimu klabu hii, wanaweza kucheza vizuri sana wana wachezaji wengi wazuri na nafikiri wanaweza kuwa juu zaidi kwenye ligi"

"Tunajua sisi ni Yanga na kila timu inataka kufanya kila kitu kushinda dhidi yetu. Wachezaji wetu wanajua hilo, na tunapaswa kufanya kila kitu kutumia jitihada nyingi kushinda mchezo huu," alisema Hamdi

Aidha Hamdi amesema wamepata wakati mzuri wa kujiandaa na mchezo huo akiwaongezea wachezaji wake mambo muhimu ya kiufundi hivyo matumaini ni kucheza vyema na kuibuka na ushindi

"Ni jambo jema kuwa na siku tano kabla ya mchezo huu, ni nafasi nzuri kwangu kuelewa wachezaji wangu vizuri zaidi"

"Nimepata muda wa kufanya marekebisho ya kiufundi mazoezini, kuweka mtazamo wangu kidogo kwa sababu si rahisi kubadilisha kila kitu mara moja"

"Wachezaji tayari wana tabia zao za uchezaji, hivyo si rahisi kubadilisha kila kitu. Nimefanya marekebisho ya kimkakati kulingana na kile ninachokiona na ninachotaka kutoka kwa wachezaji na tutaendelea kufanya hivyo kwa ajili ya kujiboresha zaidi"

"Tuna malengo mawili moja ni kupata alama tatu muhimu na jingine ni kuwashukuru mashabiki wetu waliofika kwa wingi kutupokea wametupa furaha kubwa, tumefurahi kuwaona na wamefurahia pia. Sasa ni kazi yetu kuwapa furaha kwa kushinda mchezo huu kwa ajili yao," alisema Miloud

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’