Jana Yanga ilikamilisha mechi ya raundi ya 21 kwa ushindi muhimu wa mabao 5-0 dhidi ya Mashujaa Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma
sasa Wananchi wamebakisha mechi 9 tu kukamilisha msimu lengo likiwa kutetea taji la Ligi Kuu. Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikikusanya alama 55 na kufunga mabao 55
Prince Dube na Clement Mzize wameendelea kuongoza mapambano kuelekea ubingwa wa 31 wakiwa ndio vinara wa mabao katika kikosi cha Yanga na ligi kwa ujumla
Kila mmoja amepachika mabao 10 huku Pacome Zouzoua akiwa karibu yao akipachika mabao 7 na assist 6
Dube anaendelea kuongoza waliotoa assist nyingi katika kikosi cha Yanga akiwa nazo 7 akifuatiwa na Pacome na Stephane Aziz Ki (6) ambaye pia amefunga mabao 5
Katika orodha ya nyota waliopachika mabao mengi katika kikosi cha Yanga pia lipo jina la Maxi Nzengeli aliyefunga mabao 4 na kutoa assist 5 huku beki Ibrahim Bacca nae akiingia katika orodha hiyo akiwa na mabao 4
Clatous Chama na Kennedy Musonda kila mmoja amefunga mabao 3 wakati Mudathir Yahya na Duke Abuya kila mmoja akipachika mabao 2
Kiungo Khalid Aucho jana nae akaingia katika prodha ya wapachika mabao akifunga bao lake la kwanza msimu huu akiungana na Israel Mwenda na Jean Baleke ambaye kwa sasa sio sehemu ya kikosi cha Yanga