Ni shauku kubwa ya mashabiki wa Yanga kumshuhudia winga mpya wa timu hiyo Jonathan Ikangalombo ambaye tangu ajiunge na mabingwa hao wa nchi bado hajaonekana uwanjani
Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ameweka wazi Ikangalombo anaendelea kuimarika hivyo ni suala la muda tu mashabiki watamuona
"Ikangalombo ni mchezaji mzuri naona kila mmoja ana shauku ya kumuona akicheza kwa kuwa ni mchezaji mpya"
"Hata hivyo ni muhimu kwa kila mchezaji kuwa katika kiwango bora cha utimamu 'fitness' kabla ya kuanza kucheza"
"Ni faida sio kwa timu tu, hata kwake mchezaji mwenyewe kumuepusha na changamoto za majeraha"
"Wakati akiendelea kuimarika, tutaendelea kuwatumia wachezaji ambao wako tayari kutumika, nae atakapokuwa tayari atacheza," alisema Miloud
Ikangalombo alikuwa sehemu ya wachezaji waliosafiri Kigoma katika mchezo dhidi ya Mashujaa lakini hakuwa sehemu ya wachezaji waliotumika katika mchezo huo
Lakini ni wazi, winga huyo kutoka klabu ya AS Vita anakaribia kuonekana katika uzi wa Yanga