Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kesho Jumatano kuelekea Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji ambao utapigwa Ijumaa, Februari 28 katika uwanja wa CCM Kirumba
Mabingwa hao watetezi wamepania kushinda mchezo huo ili kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo na kujiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo
Baada ya mchezo huo, March 1 Yanga itarejea Dar es salaam kujiandaa na mechi ya Derby ya Kariakoo dhidi ya Simba itakayopigwa March 08
Hivyo mchezo dhidi ya Pamba Jiji una umuhimu wa kipekee kwa Yanga ambayo inahitaji ushindi ili kwenda kucheza derby pasipo kuwa na presha
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema watakwenda Mwanza kucheza kwa tahadhari wakifahamu ubora wa Pamba Jiji lakini jambo muhimu ni kubeba alama zote tatu