Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ameanza na 'gia kubwa' timu yake ikigawa vipigo vizito katika ligi kuu ya NBC
Hamdi ameboresha pale alipoishia mtangulizi wake Sead Ramovic ambaye alitimkia CR Belouizdad ya Algeria
Mechi yake ya kwanza ilikuwa dhidi ya Ken Gold, aliishuhudia akiwa jukwaani Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 6-1 katika dimba la KMC Complex
Hamdi aliongoza rasmi mechi iliyofuata dhidi ya JKT Tanzania dimba la Meja Jenerali Isamuhyo Yanga ikilazimishwa suruhu ya bila kufungana
Baada ya mchezo huo kituo kilichofuata ilikuwa KMC, Yanga ikaibuka na ushindi wa mabao 6-1 katika dimba la KMC Complex na kisha kushinda mabao 2-1 katika uwanja huo huo dhidi ya Singida Black Stars
Hamdi akaiongoza Yanga katika mechi yake ya nne mkoani Kigoma dhidi ya Mashujaa Fc Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0
Katika mechi nne alizokaa benchi, kikosi chake kimefunga mabao 13 huku kikiruhusu mabao mawili ikiwa ni wastani wa kufunga mabao manne kila mechi
Takwimu za mechi zake za mwanzo zinaakisi kile alichosema siku alipojiunga rasmi na Yanga kuwa yeye anapenda soka la kushambulia zaidi kuliko kujilinda
Kwa sasa Yanga inashambulia na wachezaji wengi na kuwapa wakati mgumu walinzi wa timu pinzani hasa wanapopaki basi
Mpaka sasa Yanga imepachika mabao 55 katika mechi 21 zikisalia mechi 9 kuhitimisha msimu. Yanga inahitaji kufunga mabao 16 katika mechi hizo ili kufikia rekodi ya mabao 71 ya msimu uliopita
Kama vijana wa Hamdi wataendeleza kasi yao ya kufunga mabao mengi kila mechi ni wazi msimu huu wanaweza kuweka rekodi mpya ya kupachika mabao