Hamdi aandaa mkakati wa ushindi dhidi ya Pamba Jiji

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Feb 2025
Hamdi aandaa mkakati wa ushindi dhidi ya Pamba Jiji

Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema amekiandaa kikosi chake kimkakati kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Pamba Jiji ambao utapigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza

Akizungumza katika mkutano na wanahabari kuelekea mchezo huo, Hamdi alisema anatambua ubora wa Pamba Jiji pamoja na presha ambayo timu hiyo inapitia ili kujiweka salama na hatari ya kushuka daraja

"Sijui kama Pamba watacheza kwa kujilinda tu. Siwezi kuwa na uhakika kwa sababu wanahitaji alama tatu. Kama ningekuwa kocha wao, nisingetumia mbinu hiyo kwa sababu wanahitaji alama kubaki kwenye ligi.

"Timu hii imepata sare dhidi ya Singida Black Stars, jambo ambalo si rahisi. Wanaweza kushambulia na kufunga, kwa hiyo tuna mkakati wa kesho, lakini siwezi kuzungumzia hilo hapa kwa sababu ni siri ya mchezo wetu" 

"Hatujaja hapa kwa likizo. Tunaiheshimu Pamba lakini tuko hapa kushinda. Hakuna kingine zaidi ya kushinda na kupata alama tatu"

"Tunajua mchezo hautakuwa rahisi, lakini tuko tayari kupambana. Timu zote zinapocheza dhidi yetu zinatoa kila kitu. Kesho tunatarajia mchezo mgumu, lakini sisi ni Yanga, na tunapaswa kuonesha kuwa sisi ni timu kubwa," alisema Hamdi

Katika hatua nyingine, Hamdi amewapongeza mashabiki wa Yanga akiwataja kuwa mashabiki wa kipekee kutokana na kile wanachofanya kila mkoa ambako timu yao inakwenda kucheza

"Ningependa kusema kitu kuhusu mashabiki wa Yanga. Nina uzoefu mkubwa wa soka barani Afrika, nimefanya kazi na vilabu vikubwa, lakini mashabiki wa Yanga ni wa kipekee"

"Siogopi kusema hivi kwa sababu ni ukweli. Wananipa mshangao mkubwa na furaha kubwa. Wanapokuja kwa wingi kutuunga mkono, wanatupa motisha kubwa zaidi ya kupambana, kufanya kazi kwa bidii mazoezini, na kutoa kila kitu uwanjani, "alisema Hamdi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
59m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’