Kocha Mkuu wa Yanga Miloud Hamdi ameweka mkakati wa kuhakikisha anashinda mchezo unaofuata dhidi ya Simba utakaopigwa March 08 ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo
Baada ya kurejea Dar akitokea Mwanza ambapo aliiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Pamba Jiji, Hamdi amesema atatumia siku mbili kuandaa mkakati wa maandalizi kuelekea mchezo huo
Hamdi amekiri mchezo huo utakuwa mgumu kwani unazikutanisha timu bora zaidi Tanzania kwa sasa ambazo zinachuana kuwania ubingwa wa ligi kuu
Hata hivyo amesema anaamini ubora wa wachezaji katika kikosi chake unampa matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo
"Mchezo ujao, zinakwenda kukutana timu mbili bora msimu huu zinazoendelea kupishana juu ya msimamo"
"Nataka kukaa siku mbili kuwaza ni namna gani nitaingia tofauti kwenye mchezo huo mgumu. Lakini naamini wachezaji wangu watafanya kitu kikubwa, kwani Yanga tutaingia kivingine ili tupate ushindi," alisema Hamdi
Yanga ilirejea jana kutoka Mwanza ambapo Hamdi aliwapa wachezaji wake mapumziko na kesho Jumatatu wataanza maandalizi kuelekea mchezo huo
Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 58 huku watani zao Simba wakiwa nafasi ya pili na alama 54
Kama Yanga itashinda mchezo wa Jumamosi, itaongeza gap la pointi dhidi ya Simba na hivyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wakati huu ligi ikielekea ukingon