Tulieni, Yanga inakwenda kusukwa upya

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2018
Tulieni, Yanga inakwenda kusukwa upya
Kipigo cha mabao 4-0 ilichopokea Yanga usiku wa kuamkia leo kutoka kwa USM Alger, sikuwa kimewaumiza mashabiki pekee, bali ni pamoja na viongozi ambao wameapa kuisuka upya Yanga.

Aidha kipigo hicho ni mwendelezo wa matokeo duni msimu huu. Yanga imeshindwa kufikia hata nusu ya kiwango ilichokuwa nacho misimu miwili iliyopita.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na usajili ya klabu ya Yanga Hussein Nyika ni miongoni mwa viongozi walioumizwa sana na matokeo ya Yanga huko Algeria.

Nyika ndiye aliyeongoza msafara wa kikosi cha Yanga nchini Algeria wakitarajiwa kuondoka nchini humo kurejea jijini Dar es salaam leo.

Baada ya mchezo wa jana Nyika alikiri kiwango cha Yanga hakikuwa cha kuridhisha na kunahitajika mabadiliko makubwa ili kuirejesha timu katika hali ya ushindani.

Nyika amesema kwa kuanza Yanga itajaza nafasi tatu walizonazo ili kukiongezea nguvu kikosi chake huku pia wakianza mkakati wa kuisuka upya timu hiyo baada ya ligi kumalizika wiki tatu zijazo.

Katika hatua nyingine Yanga, inatarajiwa kuachana na mshambuliaji wake Donald Ngoma aliye majeruhi kwa zaidi ya miezi saba.

Kumekuwa na sintofahamu juu aina ya majeraha yanayomsumbua Ngoma.

Akihojiwa na kituo cha redio cha EFM, Nyika amesema viongozi wanakusudia kujadili mustakabali wa mchezaji huyo na watatoa taarifa siku chache zijazo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
29m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’