Ni siku tatu tu zimebaki kuelekea mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Hii ni mechi ya Wananchi, Yanga inakwenda katika mchezo huu ikiwa ni mwenyeji hivyo silaha ya kwanza inapaswa kuwa mashabiki
Mauzo ya tiketi yanakwenda kwa kasi kubwa inafahamika, kwa wale waliozoea kununua tiketi siku ya mechi huenda waipate nafasi hiyo
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametoa wito kwa Wananchi kununua tiketi zao mapema ili kuepuka usumbufu hapo baadae
Kamwe amesema hii sio mechi ya wachezaji pekee, bali ni mechi ya kila shabiki wa Yanga
ADVERTISE HERE