Tangu jana tetesi zimesambaa mitandaoni ikidaiwa kuwa Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amefungiwa miaka miwili kwa madai ya kufanya makosa ya kimaadili kinyume na kanuni za TFF
Kamwe alihojiwa siku ya Jumanne na Kamati ya Maadili ya TFF sambamba na Msemaji wa Simba Ahmed Ali ambaye Yanga ilipeleka malalamiko dhidi yake kutokana na kauli alizotoa katika moja ya mahojiano yake
Tuhuma za Kamwe zilitokana na andiko aliloweka katika ukurasa wake wa mtandao wa Instagram akihoji timu aliyoiita 'Makolo' kuwa na mfululizo wa kunufaishwa na 'makosa ya kibinadamu' ya waamuzi katika mechi zao
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Kamati baada ya kukamilisha zoezi la kuwahoji watuhumiwa lakini kusambaa mapema kwa taarifa ya Kamwe kufungiwa kunaibua maswali mengi
Kama amepatikana na hatia ingawa katika andiko lake hakutaja timu yoyote, je adhabu ya kufungiwa miaka miwili ni sawa na makosa anayotuhumiwa nayo? au lengo ni kumkomoa yeye na klabu yake ya Yanga?
Pengine pia yawezekana wale waliosambaza taarifa hiyo wana ajenda yao wakiamini wanaweza kuitoa Yanga kwenye 'focus' ya mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi
Kamwe sio mtu wa kwanza kutoa tuhuma juu ya makosa ya kibinadamu ya waamuzi ambayo yameinufaisha sana timu ile msimu huu
Mijadala imekuwa mingi, na ushahidi wa matukio hayo upo sasa badala ya kufanya uchunguzi kujiridhisha na kuchukua hatua, tunaona ni sawa kuwaadhibu wale wanaosema ukweli?
Yanga na Simba ni timu wapinzani, lakini pia timu hizi ni watani wa jadi. Kama ni kauli za 'kuudhi' naamini msemaji wa Simba Ahmed Ali anaweza kuwa kinara kwa kutoa kauli za aina hiyo
Lakini hata siku moja hakuwahi kuhojiwa na Kamati, kilichompelekea kuhojiwa safari hii ni baada ya Yanga kupeleka malalamiko dhidi yake
Ikitokea Kamwe amefungiwa nafikiri hatua hiyo haitaungwa mkono Wanayanga na itapeleka presha kubwa kwa wenye mamlaka