Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kusahau kilichotokea Jumamosi na wajitokeze kwa wingi kesho Jumatano kuishangilia timu yao katika mchezo wa kombe la Shirikisho la CRDB dhidi ya Coastal Union
Yanga itakuwa mwenyeji wa Coastal Union katika mchezo wa hatua ya 32 bora kuwania tiketi ya kutunga hatua ya 16 bora
Kamwe amesema anajua mashabiki wana kiu kubwa ya kuiona na kupata burudani kutoka kwa timu yao, vijana wako tayari kuwapatia burudani hiyo
"Timu yetu inaendelea vyema na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Coastal Union. Tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi uwanja wa KMC Complex siku ya Jumatano kuipa sapoti timu yao"
"Najua wengi wana shauku kubwa ya kuiona timu ikicheza baada ya kipindi kirefu kupita. Viingilio vilitangazwa mapema VIP ni Tsh 20,000/- na Mzunguuko ni Tsh 10,000/-"
"Wachezaji wetu walipata nafasi ya kufanya mazoezi uwanja wa KMC Complex siku ya Jumatatu na leo tutakamilisha maandalizi yetu Avic Town," alisema Kamwe