Jana GSM Foundation kwa kushirikiana na Hospitali ya CCBRT na klabu ya Yanga waliendesha Harambee ya Mwezeshe atembee kwa ajili ya kukusanya fedha ili kutibu watoto 400 wenye Mguu Kifundo, kimombo ClubFoot katika Hospitali bingwa ya CCBRT
Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dr. Emmanuel Nchimbi aliambatana na Mufti mkuu wa Bakwata, Dr. Abubakar Bin Zubeir waliungana na Ghalib Said Mohamed ambaye Taasisi yake ndio iliyoandaa tukio hilo kubwa
Zaidi ya Tsh 1B zilikusanywa na kuvuka malengo ya kukusanya Tsh 600M fedha ambazo ndizo zilizohitajika kwa ajili ya matibabu ya watoto hao
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema fedha hizo zitakwenda kuhudumia watoto wenye Mguu Kifundo ambapo takribani watoto 2,000 huzaliwa kila mwaka nchini Tanzania wakiwa na taatizo hilo
"Watoto hawa wakipata matibabu wataepuka kilema cha milele na wakikosa matibabu ni kinyume chake, ulemavu wa milele. Shujaa wetu Dr. Brenda Msangi, CEO wa Comprehensive Community Based Rehabilitation Tanzania (CCBRT) ataendesha jahazi hili la MWEZESHA ATEMBEE," alisema Hersi
Katika Harambee hiyo GSM alichangia Tsh Milioni 100 huku picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ikiuzzwa Tsh Milioni 104
Picha hiyo ilinunuliwa na Wizara ya Afya, Benki ya NMB, Benki ya CRDB pamoja na Katiby ya CCM Dkt. Emanuel Nchimbi

Lakini pia jezi ya Yanga iliuzwa Tsh Milioni 35 huku wachezaji Stephane Aziz Ki, Dickson Job na Kibwana Shomari wakiwa miongoni mwa waliochangia Harambee hiyo kila mmoja akichangia Tsh Milioni 7