Hamdi afunguka mwanzo wa Ikangalombo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Mar 2025
Hamdi afunguka mwanzo wa Ikangalombo

Baada ya winga Jonathan Ikangalombo kuonyesha uwezo wake ndani ya dakika 66 alizopewa, kocha mkuu wa Yanga Miloud Hamdi amesema nyota huyo ameanza vyema majukumu yake lakini bado atahitaji muda zaidi

Ikangalombo aliyetua Yanga dirisha dogo la msimu huu, amecheza mechi mbili, moja ya ligi dhidi ya Pamba Jiji na alipewa dakika 21 kisha dakika 45 dhidi ya Coastal Union katika Kombe la FA.

Ni wazi, kiwango cha winga huyo taratibu kimeanza kumvutia Hamdi, japokuwa bado hajafunga wala kutengeneza nafasi ya bao

Hamdi amesema, Ikanga ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na kwa sasa ndio anaingia kwenye kikosi hivyo hana haraka ya kumwona akifanya makubwa

"Ameanza vyema lakini nadhani bado anahitaji kuzoeana na wenzake, lazima wenzake wajue anahitaji pasi za aina gani ili kuisadia timu kupata matokeo mazuri"

"Pia anatakiwa kuingia kwenye mifumo ya timu na azijue falsafa zake, kuhusu kufunga nimemwambia sitaki aweke akilini sana jambo hilo kwani ishu hiyo siyo kazi yake kubwa, mabao yatakuja tu"

"Sitaki afanye vitu kwa presha ya mashabiki, naamini baada ya miezi michache Ikanga atakuja kuwa mchezaji tegemeo kwenye timu na hatari kwenye ligi," Hamdi alinukuliwa na Mwanaspoti

Ikangalombo mbali na kucheza winga zote mbili, kulia na kushoto, pia ana uwezo wa kutumika kama mshambuliaji wa kati

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
3h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
7h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’